Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida
(Hospitali ya Mkoa)

HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA SINGIDA YATOA MAFUNZO YA MAADILI YA UUGUZI KWA WAUGUZI WOTE

Posted on: February 25th, 2022

Mafunzo hayo ya Maadili ya Uuguzi yametolewa kwa muda wa siku 5 kuanzia tarehe 21.02.2022 hadi tarehe 25.02.2022 ambapo takribani wauguzi 270 wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida Wamefanikiwa kupata mafunzo hayo.


Wakiongea baada ya mafunzo hayo wauguzi walioshiriki mafunzo hayo, wamesema, wamefurahi sana kupatiwa mafunzo hayo ya Maadili ya Uuguzi mbayo yametolewa na Wauguzi Nguli kutoka Baraza la Wauguzi Tanzania, pia wauguzi hao wameahidi kufanya kazi zao kwa kuzingatia Maadili yote ya Uuguzi na wamemuahidi Mganga Mfawidhi kwamba hatosikia malalamiko yoyote kutoka kwa wagonjwa yanayowahusu Wauguzi.