HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA SINGIDA YATOA MAFUNZO YA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZWA KWA WATUMISHI WAKE WOTE
Posted on: December 4th, 2021Mafunzo hayo ya magonjwa yasiyoambukizwa yametolewa kwa muda wa siku 5 kuanzia tarehe 30/11/2021 hadi tarehe
04/11/2021 ambapo takribani watumishi 320 wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida Wamefanikiwa kupata mafunzo
hayo.
Wakiongea baada ya mafunzo hayo watumishi walioshiriki mafunzo hayo wamesema, wamefurahi sana mafunzo hayo
kutolewa kwa watumishi wote kwani mbali na kupata mafunzo juu ya udhibiti wa magonjwa yasiyoambukizwa washiriki
walisema wamepata fursa ya kujifunza namna ya kukabiliana na Ukimwi mahala pa kazi, namna ya kujikinga na ugonjwa
wa Corona, umuhimu wa kupata chanjo ya korona, umuhimu wa kutowanyanyapaa wagonjwa wa Ukimwi. Pia washiriki
walisema wamejifunza juu ya Haki na Wajibu wa Mtumishi wa Umma. Washiriki wa mafunzo haya wamesema elimu
waliyoipata watahakisha wanaitoa kwa watumishi wenzao hususani watumishi wa ajira mpya watakaokuwa wanapangiwa
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida bila kuzisahau familia zao.