KATIBU MKUU (AFYA) ATEMBELEA HOSPITALI YA RUFAA SINGIDA
Posted on: October 19th, 2019Na Emmanuel J. Borra,
Katibu Mkuu (Afya) Dkt. Zainab Chaula amesema tumepata kiasi cha Bilioni 1.5 za kuazia ujenzi wa wodi ya wagonjwa hospitali ya rufaa ya mkoa Singida. Ameyasema hayo alipoitembelea hospitali hiyo tarehe 16 Oktoba 2019 baada ya kukagua msingi wa jingo hilo ambalo ujenzi wake umesimama kwa muda mrefu.
Katika maelezo yake katibu mkuu amesema “Lengo letu nimekuja na timu nzima ya wakurugenzi, ni namna gani tunakusanya nguvu ya kiusimamizi, nashukuru wadau na serikali tumepata pesa Bilioni 1.5 za kuanzi na zipo tayari kwa hiyo nimekuja kuona ni namna gani tunatembea pamoja kwa maana ya usimamizi na pia kupeana moyo.”
Awali akizungumza na watumishi aliwaeleza kuwa yupo njiani kuelekea Mwanza na kwaajili ya ziara ya kikazi lakini Singida ni njiani hivyo amepitia ili kuwasalimia na kuwatia moyo. Aidha amewataka watumishi kufanya kazi kwa bidii na kuongeza makusanyo ya hospitali na kuwahudumia wagonjwa.
Hospitali ya mkoa Singida ilijengwa mwaka 1954 ambapo kwa kipindi hicho idadi ya wakazi ilikuwa 300,000. Kulingana na Sensa ya 2002 idadi ya wakazi imeongezeka kufikia wakazi 1,090,948 na kufikia sasa kuna jumla ya wakazi 1,294,584. Wakazi hawa wote wanategemea huduma za hospitali hii ambapo kimsingi haitoshelezi huduma wanayohitaji wakazi hawa wote. Kasi ya wagonjwa imeongezeka na kwa kuzingatia sera ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ya mwaka 2007 kwamba kila mkoa uwe na hospitali yake ya rufaa uongozi wa mkoa kwa kushirikiana na wananchi waliamua kujenga Hospitali mpya ya Rufaa ili kuendana na mahitaji ya sasa. Aidha kwa kifupi sababu za kujenga hospitali mpya ni pamoja na Ongezeko la wagonjwa, eneo dogo ilipo hospitali ya sasa hekta 1.5, uchakavu wa miundombinu ya majengo, maji na umeme, kukosekana kwa idara muhimu na vifaa ili kutoa huduma bora za kibingwa, utekelezaji wa sera ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Ujenzi wa Hospitali mpya ya rufaa unagharimiwa na serikali kwa asilimia 100 ulianza rasmi mwaka 200/2009 ambapo mkandarasi wa kwanza alikuwa ni kampuni ya China Civil Engineering and Construction Company Ltd chini ya mhandisi mshauri ambaye ni chuo kikuu cha Ardhi.
Kufikia tarehe 30/12/2019 baadi ya huduma zilianza kutolewa ambazo ni kliniki ya afya ya uzazi na mtoto, Huduma ya tiba kwa wagonjwa wa nje, kliniki ya magonjwa ya ngozi na kliniki ya kisukari. Kufikia sasa baadhi ya majengo yamekamilika na huduma zingine zilihamishiwa na zinaendelea kutolewa katika hospitali mpya rufaa ambapo kukamilika kwa ujenzi wa jingo jipya la wodi kutawezesha huduma zote kuhamishiwa hospitali mpya.
Akizungumza katika ziara hiyo mganga mkuu wa mkoa Dkt. Victorina Ludovic amesema ni changamoto kubwa kuendesha hospitali mbili kwa mara moja kwa kuwa hospitli ya zamani iko mjini nah ii mpya ipo Mandewa na idadi ya watumishi ni ile ile na kwa mujibu wa ikama idadi ya watumishi ni chini ya asilinia hamsini lakini paoja na upungufu huo amewapongeza watumishi kwa kufanya kazi kwa bidii. Dkt. Victorina ameshukuru ujio wa ziara hii kwakuwa tumepatia fedha za ujenzi wa hospitali mpya na ile ya zamani watapewa manispaa na kuwa hospiatli ya wilaya.