Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida
(Hospitali ya Mkoa)

KATIBU TAWALA MKOA WA SINGIDA AMPONGEZA MGANGA MFAWIDHI HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA SINGIDA

Posted on: January 6th, 2022

Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt. Doroth Mwaluko amempongeza Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida kwa kufanikisha sherehe ya Siku ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida. Sherehe ya Siku ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida imefanyika tarehe 08/01/2022 na kila tarehe 08 Januari sherehe hii ya siku ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida itakuwa inafanyika. Sherehe hizi ziliambatana na Bonanza ambapo Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida walishiriki michezo mbalimbali kama vile mpira wa miguu, mpira wa kikapu, kuruka kamba, riadha, shindano la kula chakula katika uwanja wa maonyesho Mandewa. Pia wananchi walipata fursa ya kupima chanjo ya Uviko 19, kupima presha, kupima uzito, kupima urefu, kupima sukari, kupima macho, kuchangia damu na ushauri nasaha. Huduma zote hizi wananchi walipatiwa bure.