Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida
(Hospitali ya Mkoa)

UZINDUZI WA BODI YA HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA SINGIDA.

Posted on: December 27th, 2024


Akifungua hafla hiyo ya uzinduzi wa bodi ya Hospitali uliofanyika mapema leo tarehe 28 Disemba 2025 Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Bi Halima Omary Dendego ameipongeza serikali ya awamu ya sita ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya katika sekta ya Afya kwa kuendelea kuwa nayo bega kwa bega kusapoti huduma bora za Afya.


Ameendelea akiwapongeza wajumbe wa Bodi hiyo ambayo imeundwa na wajumbe kumi (10) na katiyao Mwenyekiti akiwa Ni Bi Safina Muhindi na katibu wake akiwa Ni Dkt. David J Mwasota (Mganga Mfawidhi wa Hospitali) kwa kuanza na mafunzo ya bodi hiyo itakayo hudumu kwa muda wa Miaka mitatu kwani mafunzo hayo yamewaleta pamoja wajumbe kuweza kujenga ushirikiano ambao Ni wa muhimu sana katika utendaji kazi wao wa kilasiku. 

Amewaomba wajumbe wa bodi wafanye kazi kwa ufasaha na kwa ushirikiano na uwajibikaji wa hali ya juu ili kuifanya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida izidi kufanya vizuri katika utoaji wa huduma bora kwa Watanzania kama ilivyo kauli mbiu ya Hospitali hiyo “huduma bora ni kipaumbele chetu”


Akifunga hafla hiyo ya uzinduzi wa bodi ya Hospitali  ya Rufaa Mkoa wa Singida  amempongeza Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Victorina Ludovick amepongeza uongozi wa Hospitali kwa ujumla kwa ushirikiano wa karibu katika kuhakikisha wanasingida na watanzania wote wanapata huduma bora za Afya.

Mwisho kabisa ameishukuru bodi hiyo na kuitakia kila lakheri katika utendaji wa majukumu ya bodi na kuwakabidhi miongozo itakayowaongoza katika shughuli zao kama bodi ya Hospitali.