WANAFUNZI WA CHUO CHA UHASIBU SINGIDA WAITEMBELEA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA SINGIDA.
Posted on: January 28th, 2022Leo tarehe 29.01.2022 Wanafunzi wa chuo cha uhasibu Singida kutoka kikundi cha “charity concert” wameitembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida na kufanya usafi maeneo mbalimbali ya Hospitali. Pia wanafunzi hao wameto misaada mbalimbali kwenye wodi ya kina mama wajawazito pamoja na Watoto.
Akiongea baada ya kutoa misaada hiyo Katibu wa “Charity Concert” bwana Edmund T. Mwambashi alisema kwamba utaratibu huu wa kuwaona watu wenye shida mbalimbali katika kikundi chao hufanyika kila mwanzo wa semista na mwisho wa semista.