Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida
(Hospitali ya Mkoa)

FAHAMU KUHUSU UGONJWA WA EBOLA NA JINSI YA KUJIKINGA

Posted on: November 28th, 2019

UTANGULIZI    

Ugonjwa wa Ebola ni ugonjwa wa hatari unaosababishwa na virusi vya Ebola. Ugonjwa huu ni miongoni mwa magonjwa ya milipuko yajulikananyo kama homa za virusi vinavyosababisha kutoka damu mwilini

Ugonjwa huu kwa asili upo kwa wanyama kama vile nyani, sokwe na popo. Ugonjwa wa Ebola huambukizwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu au binadamu kwa binadamu mwingine kwa haraka.

JINSI UGONJWA WA EBOLA UNAVYOAMBUKIZWA TOKA KWA WANYAMA KWENDA KWA BINADAMU

Binadamu anapata virusi vya Ebola kwa kula au kugusa viungo na majimaji ya wanyama pori wenye maambukizi ya ugonjwa huo.

JINSI  UGONJWA WA EBOLA UNAVYOAMBUKIZWA MIONGON MWA JAMII

Virusi vya Ebola huenea kwa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine kwa njia zifuatazo:

 1. kugusa majimaji ya mwili kama vile damu, matapishi, jasho,mate,machozi, mkojo au kinyesi kutoka kwa mtu aliyeambukizwa ugonjwa huu.
 2. kugusa au kuosha maiti ya mtu aliyekufa kwa ugonjwa wa Ebola
 3. kugusa vyombo na nguo zilizotumiwa na mtu mwenye maambukizi ya Ebola
 4. kichangia vitu vyenye ncha kali na mtu mwenye maambukizi ya ugonjwa wa Ebola

NB: Ugonjwa huu hauenezwi kw anjia ya hewa

DALILI ZA UGONJWA WA EBOLA

Dalili za ugonjwa wa ebola huanza kijitokeza kwa mtu aliyeambukizwa virusi hivi kuanzia siku 2 hadi 21 tangu kupata maambukizi. Dalili hizo ni pamoja na:

 1. Homa kali ya ghafla
 2. Kulegea kwa mwili
 3. Maumivu ya misuli
 4. Kuumwa kichwa na vidonda kooni
 5. Mara nyingi dalili hizo hufuatiwa na kutapika, kuhara na vipele vya ngozi
 6. Kwa baadhi ya wagonjwa kutokwa damu sehemu za wazi za mwili kama vile kwenye macho, pua, masikio, mdomo na njia za haja kubwa

MATIBABU

Ugojwa wa ebola huana tiba wala chanjo, bali mgojwa hutibiwa kulingana na dalili zitakazo ambatana na ugonjowa huo. Kuna uwezekano mkubwa wa kuepuka kupoteza maisha iwapo mgonjwa huyo atawahi kupata huduma satahiki.

JINSI YA KUJIKINGA NA UGONJWA WA EBOLA

Ugonjwa wa ebola unaweza kuzuilika kwa kuzingatia yafuatayo;

 1. Epuka kugusa damu, matapishi, kamasi, mate, machozi, mkojo, kinyesi na majimaji mengiine yanayotoka mwilini mwa mtu mwenye dalili za ebola.
 2. Epuka kugusa au kuosha maiti ya mtu aliyekufa akiwa na dalili za Ebola, toa taarifa kwenye kituo cha huduma za afya.
 3. Epuka kutumia nguo, matandiko, kitanda, godoro na vyombo vilivyotumika na mtu mwenye dalili za Ebola.
 4. Epuka kugusa wanyama kama vile popo, nyani sokwe, tumbili, swala au mizoga ya wanyama.
 5. Zingatia ushauri na maelekezo yanayotolewa na wataalam wa afya na viongozi wa serikali
 6. Wahi kituo cha kutolea huduma za afya unapohisi mojawapo ya dalili za ugonjwa wa Ebola.
 7. Toa taarifa mapema kwenye kituo cha huduma za afya au kwa viongozi wa serikali ya mitaa, kijiji au kata mara uonapo mtu mwenye dalili za Ebola.

KUMBUKA:

Kunawa mikono mara kwa mara kwa sabuni na maji yanayotiririka ili kujikinga na ugonjwa wa Ebola.