BODI YA USHAURI YA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA SINGIDA YAFANYA KIKAO CHAKE CHA ROBO YA PILI KWA MWAKA 2025/2026.
Posted on: February 6th, 2026Leo tarehe 07 Februari, 2026, Bodi ya Ushauri ya Hospitali ya Rufaaa ya Mkoa wa Singida imefanya kikao chake cha robo ya pili kwa mwaka 2025/2026 katika Ukumbi wa Tiba Mtandao. Kikao hicho kimefunguliwa na Mwenyekiti wa Bodi Bi. Safina S. Muhindi, kwa kuwakaribisha wajumbe wa Bodi pamoja na sekretarieti katika kikao hicho.

Mganga Mfawidhi Dkt. Muhaj M. Kamtande amewasilisha taarifa ya miradi mbalimbali inayoendelea hospitalini hapo na kueleza kuwa miradi hiyo inaendelea kwa kasi nzuri na inatarajiwa kukamilika ndani ya muda uliopangwa. Miongoni mwa miradi hiyo ni:
Mradi wa Kusafisha Figo (Dialysis),
Mradi wa Jengo la Watoto Wachanga (NICU) pamoja
na Mradi wa Jengo la Damu Salama.

Aidha, kikao hicho kimejadili pia mambo mbalimbali ikiwemo taarifa ya watumishi kwa kipindi cha Oktoba–Desemba 2025, taarifa ya utekelezaji wa maazimio ya kikao kilichopita, taarifa ya mkaguzi wa ndani, hali ya upatikanaji wa dawa, taarifa ya utekelezaji wa shughuli zilizopangwa kwenye mpango kabambe wa hospitali (CHOP) pamoja na taarifa ya viashiria vya uboreshwaji wa huduma katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida.
Baada ya majadiliano, wajumbe wa Bodi walifanikiwa kutembelea miradi hiyo na kujionea hatua za utekelezaji.

Mwisho, Bi. Safina S. Muhindi alifunga kikao kwa kuwashukuru wajumbe kwa ushiriki wao na kuwasihi waendelee kuchapa kazi kwa bidii ili kuleta maendeleo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida.


