BODI YA USHAURI YA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA SINGIDA YAFIKA DODOMA RRH.
Posted on: April 10th, 2026Wajumbe hao nane pamoja na sekretariet ya bodi hiyo ya ushauri ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida wamefika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kubadilishana uzoefu juu ya namna ya kuendesha bodi, namna ya kutoa huduma bora kwa Watanzania na namna ya kuweka vizuri mazingira yote ya hospitali.

Akizungumza baada ya ziara hiyo Mwenyekiti wa bodi ya ushauri ya Singida RRH Bi Safina Muhindi ameipongeza bodi ya ushauri ya Dodoma RRH kwa kuwa na ushirikiano mkubwa na menejimenti ya Dodoma RRH pamoja na watumishi wote.
Nae Mganga Mfawidhi wa Singida RRH Dkt. Muhaji M. Kamtande alisema malengo ya ziara hiyo yamefanikiwa kwa asilimia 100%.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Victorina Ludovick alisema "Tumetembelea maeneo karibia yote ya kutolea huduma hapa Dodoma RRH kwa kweli watumishi wanaonekana kuwa ni watu wanaowajibika kwa mujibu wa STK pia wapo nadhifu kwelikweli ".



