Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida
(Hospitali ya Mkoa Mandewa)

HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA SINGIDA (SINGIDA RRH) YATEMBELEA BOHARI YA DAWA (MSD) DODOMA OKTOBA 17, 2025 LENGO KUU LIKIWA NI KUENDELEA KUDUMISHA NA KUBORESHA ZAIDI UHUSIANO MZURI KATI YA SINGIDA RRH NA BOHARI YA DAWA (MSD).

Posted on: October 15th, 2025

Akifungua kikao hicho Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida Dkt. Muhaj K. Mohammed ameishukuru timu ya MSD kwa mapokezi mazuri na kwa kazi wanayo ifanya katika kulijenga Taifa.


Akiendelea kwa kueleza dhumuni la ugeni huo ikiwa  Ni kudumisha na kuboresha zaidi uhusiano Kati ya Singida RRH na MSD katika utoaji wa huduma za Afya kwa Watanzania kwa ujumla.

Aidha Dkt. Muhaj ameisisitiza timu ya MSD  juu ya  kuendelea kuzingatia Ubora wa vifaa tiba pamoja na dawa. 

Timu yote ya Singida RRH ili unga mkono hoja ya Dkt. Muhaj kwa kusisitiza ubora wa huduma zinazotolewa na MSD uendelee kuzingatiwa ili kuhakikisha Watanzania wanapata matibabu katika mazingira yaliyobora.

Nae Afisa Huduma kwa Mteja kutoka MSD Dodoma Bi. Juliana Mbogo ameishukuru timu ya uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida kwa kufika Bohari ya dawa Mkoani Dodoma.

Amewahakikishia juu ya kuendelea kuzingatia Ubora wa huduma wanazo zitoa ambazo ni kuhakikisha kila eneo la kitaalam linapata dawa zenye ubora na vifaa tiba vilivyo bora kwa wakati mfano; Vifaa vya Maabara, vifaa vya Upasuaji na vingine vyote vinavyo husika katika ufanikishaji wa huduma za Afya kwa ujumla.


Vile vile timu zote mbili kutoka Bohari ya dawa MSD Dodoma na timu kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida baada ya Kikao kifupi wametembelea sehemu vifaa tiba na dawa