Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida
(Hospitali ya Mkoa Mandewa)

KLINIKI TEMBEZI YA KIBINGWA BOBEZI YA MAGONJWA YA MOYO | 1-5 DISEMBA 2025

Posted on: December 4th, 2025

Katika kipindi cha siku tano kuanzia tarehe 1 hadi 5 Disemba 2025, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida (Singida RRH) ilifanikiwa kuendesha kliniki tembezi ya kibingwa Bobezi ya magonjwa ya moyo, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kusogeza huduma za kibingwa Bobezi karibu na wananchi.



Jumla ya wagonjwa 179 walipatiwa huduma za uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo, wakiwemo watu wazima 154 na watoto 25. Kati yao, wagonjwa 127 waligundulika kuwa na changamoto za magonjwa ya moyo na kuanza kupatiwa matibabu stahiki. Aidha, wagonjwa 29 waliandikiwa rufaa kwa ajili ya uchunguzi wa kina na matibabu ya kibingwa zaidi, ikijumuisha watu wazima 15 na watoto 14.


Utekelezaji wa kliniki hii umeendelea kuthibitisha dhamira ya Singida RRH katika kuboresha upatikanaji wa huduma bora za afya, hususan huduma za kibingwa Bobezi na kuhamasisha wananchi kuwahi hospitalini kwa uchunguzi wa mapema.