MAFUNZO YA HUDUMA BORA KWA MTEJA (CUSTOMER CARE) | SRRH – SINGIDA
Posted on: February 17th, 2026Leo Februari 18, 2026, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida (SRRH) imefanya mafunzo ya Huduma Bora kwa Mteja (Customer Care) yakiongozwa na Bi. Yolanda Urio, Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Mteja – Benki ya CRDB.

Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida, Dkt. Muhaj M. Kamtande, alimkaribisha mgeni rasmi pamoja na watumishi wote na kusisitiza umuhimu wa mafunzo hayo katika utendaji wa kazi wa kila siku, hususan namna bora ya kuwasiliana na wagonjwa/wateja, kuwa makini, kujifunza zaidi na kuimarisha weledi katika utoaji wa huduma.

Kwa upande wake, Mgeni Rasmi Mganga Mkuu wa Mkoa, Dkt. Victorina Ludovick, amewapongeza watumishi kwa kujitokeza na kusisitiza kuwa yote watakayojifunza yawekwe katika vitendo. Pia amewakumbusha watumishi kumuunga mkono Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuleta tabasamu kwa wagonjwa kupitia huduma zenye utu, upendo na ukarimu.

Amemalizia kwa kuwakumbusha kauli mbiu ya Hospitali isemayo “huduma bora ni kipaumbele chetu”


