Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida
(Hospitali ya Mkoa Mandewa)

MGANGA MKUU WA MKOA WA SINGIDA AFUNGA MAFUNZO YA HUDUMA BORA KWA MTEJA SRRH.

Posted on: February 18th, 2026

Akifunga mafunzo hayo ya Huduma Bora kwa mteja yaliyofanyika kwa muda wa siku mbili Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Victorina Ludovick alimpongeza Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida Dkt. Muhaj M. Kamtande kwa kuratibu mafunzo hayo ya siku mbili ambayo yalihudhuriwa na watumishi zadi ya 500 wa kada mbalimbali kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida.


Dkt. Victorina aliwasisitiza washiriki wote wa mafunzo hayo kuhakikisha baada ya mafunzo hayo kunakuwa na mabadiliko makubwa sana kwenye idara zote za Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida kwa kuhakikisha huduma zinatolewa kwa wakati, kuhakisha watu wote wanaofika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida wanatoka hapo huku wakiwa wanatabasamu kutokana na huduma nzuri watakayopatiwa Hospitalini hapo.