Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida
(Hospitali ya Mkoa Mandewa)

TUMAINI JIPYA KWA WAGONJWA WA HEMOFILIA

Posted on: April 16th, 2026

Aprili 17, 2026, maadhimisho ya Siku ya Hemofilia Duniani kitaifa yamefanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida, yakiongozwa na Mganga Mkuu wa Mkoa, Dkt. Victorina Ludovick aliyemwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya.


Akizungumza katika maadhimisho hayo, Dkt. Victorina amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Serikali na wadau katika kupambana na hemofilia, huku akibainisha hatua zilizofikiwa ikiwemo kuanzishwa kwa kanzi data ya wagonjwa na utoaji wa vitambulisho ili kuboresha huduma.


Aidha, Dkt. Victorina amesema kuwa mafunzo yametolewa kwa watoa huduma ngazi ya jamii, waganga wa tiba asili na wataalamu wa afya ili kuongeza uelewa na kuwabaini wagonjwa mapema.

Vilevile, Dkt. Victorina amebainisha kuwa kliniki za hemofilia zimeanzishwa katika hospitali 15 nchini na wagonjwa zaidi ya 500 pamoja na walezi wao wamepatiwa elimu ya namna ya kuishi na ugonjwa huo.


Kwa upande wa jamii, Dkt. Victorina amesisitiza kuondoa dhana potofu kuhusu hemofilia kupitia elimu sahihi ili kupunguza unyanyapaa na kuboresha upatikanaji wa huduma.

Maadhimisho haya yameleta matumaini mapya kwa wagonjwa wa Hemofilia Nchini