Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida
(Hospitali ya Mkoa Mandewa)

USHIRIKIANO WAENDELEA KUIMARIKA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA SINGIDA

Posted on: May 10th, 2026

Wageni kutoka Compassion International wakiongozwa na Dkt. Michael kutoka NetherLands leo wametembelea huduma mbalimbali zinazotolewa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida ikiwa ni sehemu ya kuendelea kuimarisha mahusiano na ushirikiano kuelekea mbio za hisani zitakazofanyika Mkoa wa Singida.


Katika ziara hiyo, wageni hao wamepata fursa ya kujionea ubora wa huduma za matibabu, matumizi ya vifaa tiba vya kisasa pamoja na maendeleo makubwa ya miundombinu ya afya yanayoendelea kufanywa na Serikali katika kuboresha Sekta ya Afya nchini.


Aidha, wageni hao wamepongeza juhudi zinazofanywa na hospitali hiyo katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora, salama na zenye viwango vya kisasa.