Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida
(Hospitali ya Mkoa Mandewa)

WAUGUZI WATARAJALI WAAGWA RASMI MAPEMA LEO NOVEMBA 6, 2025 BAADA YA KUMALIZA MUDA WA MAFUNZO YA VITENDO HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA SINGIDA.

Posted on: November 6th, 2025

Akifungua Hafla hiyo mgeni rasmi Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida Dkt. Muhaj K. Mohamed amewapongeza Wauguzi Watarajali kwa kumaliza muda wao wa Mafunzo ya vitendo Salama bila changamoto zozote. 

Amewasisitiza juu ya kwenda kuzingatia utoaji wa huduma bora kwa Watanzania, kuwajali na kuwathamini wagonjwa (Customer Care). Amewasisitiza kuwa mgonjwa Ni Kipaumbele kwa mtoa huduma hivyo wakatoe Kipaumbele kwa wateja kule wanapoenda kutoa huduma baada ya mafunzo ya vitendo.

Sambamba na hilo amewakumbusha 

 kuzingatia mawasiliano na mteja na kusema kuwa mawasiliano na mteja lazima yawe mazuri na yenye staha pamoja na nidhamu katika utendaji kazi wao wa kila siku.

Aidha Muuguzi Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida Bi. Theresia P. Ntui amewaasa juu ya kuzingatia Maadili ya Utumishi wa Umma, kuepuka makundi mabaya pale wanapoingia kazini baada ya Kumaliza mafunzo ya vitendo.

Nae Muuguzi Mkuu wa Mkoa Bi Hyasintha Alute amewapongeza pia wauguzi watarajali kwa kumaliza muda wao wa mafunzo ya vitendo kwani ni hatua kubwa sana.

Bi. Hyasintha alieleza vitu vya muhimu anavyopaswa Muuguzi kuzingatia katika taaluma yake ya Uuguzi ambavyo ni Usiri wa taarifa za wagonjwa na Wafanye kazi kama wataaluma, na wafanye  kazi zao kwa usawa bila kubagua wagonjwa. 

Amemaliza kwakusema “Mkatende haki kwa Wagonjwa na mkafanye kazi kwa bidii haijalishi mazingira mnayofanyia kazi yapoje.