Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida
(Hospitali ya Mkoa)

HUDUMA YA MATIBABU YA MACHO YAHAMISHIWA

Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida anapenda kuwatangazia wakazi wa Singida na wananchi wote kwa ujumla  

kuwa kwa sasa huduma ya matibabu ya macho inapatikana katika Hospitali yetu mpya ya Rufaa iliyopo eneo la Mandewa. Kwa sasa 

huduma hiyo haipatikani katika Hospitali ya zamani iliyopo mjini karibu na ofisi za posta Singida. 

Ikiwa unahitaji huduma hii ya matibabu ya macho tunashauri uje moja kwa moja Hospitali mpya ya Rufaa iliyopo Mandewa ili kuepuka usumbufu.

Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.


- 18 November 2019