Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida
(Hospitali ya Mkoa)

MATIBABU YA MENO, MACHO NA HUDUMA KWA WAGONJWA WA NJE SASA ZINAPATIKANA MANDEWA

Mganga mafawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Singida anapenda kuwatangazia wananchi wote kuwa huduma za matibabu ya meno, 

matibabu ya macho na huduma kwa wagonjwa wa nje sasa zinapatikana katika Hospitali yetu mpya ya Rufaa iliyopo eneo la Mandewa.

Huduma ya matibabu ya meno na huduma ya matibabu kwa wagonjwa wa nje zinapatikana katika hospitali zetu zote mbili (Iliyopo mijini na iliyopo Mandewa).

 Huduma ya matibabu ya macho inapatikana katika Hospitali mpya ya Rufaa iliyopo Mandewa tu kama tulivyotangaza hapo awali.

- 18 November 2019