Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida
(Hospitali ya Mkoa)

KLINIKI ZA TIBA USINGIZINI NA GANZI (ANAESTHESIA CLINIC)

Posted on: December 6th, 2023

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida tunaendesha kliniki za tiba usingizini na ganzi kwa siku zote za Juma. Kliniki hii inaendeshwa na Daktari Bingwa wa Tiba Usingizini na Ganzi (Anaesthesiologist).

Tunaona wagonjwa wote wanaopangiwa kufanyiwa upasuaji kabla na baada ya upasuaji. Pia tunashirikiana na idara ya matibabu ya viungo (Physiotherapy) kuendesha kliniki kwa wagonjwa wenye maumivu ya muda mrefu (Chronic pain).