Nafikaje Singida RRH
Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Singida inafanya shughuli zake za matibabu kata ya Mandewa;
Unaweza kufika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida iliyoko kata ya Mandewa kwa kutumia usafiri binafsi, wa umma au wa kukodi.
- Kwa kutumia usafiri wa umma Hospitali ya Rufaa ya Mkoa inafikika vizuri kwa madereva hasa wa BAJAJ na Piki piki (Boda boda) hivyo mueleze dereva uendako nae atakufikisha.
- Kwa kutumia usafiri binafsi ili kufika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, ukiwa unatokea mjini kati, fuata barabara ya Mwanza na ufikapo sheli ya Nassco elekea barabara ya Sepuka (Barabara inayo elekea upande wa kushoto) moja kwa moja umbali wa 3.88 Km (2.41 Mi) kutoka makutano hayo ya barabara paka utakapo ona kibao cha Hospitali ya Rufaa Mandewa. Na ukiwa umetokea Bomani basi fuata barabara ya Bomani kuelekea sheli ya Nassco kisha uelekee na barabara ya kwenda sepuka moja kwa moja umbali wa 3.88 Km (2.41 Mi) kutoka makutano hayo ya barabara mpaka utakapo ona kibao cha Hospitali ya Rufaa ya Mkoa.