GARI JIPYA LA WATUMISHI LAZINDULIWA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA SINGIDA
Posted on: November 30th, 2021Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Beneth Mahenge azindua rasmi gari la Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa
Singida.
Uzinduzi huo wa gari la Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida umefanyika leo tarehe 30/11/2021 katika
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida eneo la Mandewa ambapo Mkuu huyo wa Mkoa wa Singida alizindua rasmi gari la
watumishi wa Hospitali ya Rufaa mpya aina ya Coaster ambayo imenunuliwa na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida
kwa mapato ya ndani.
Akiongea katika uzinduzi huo Daktari Mahenge alisema kwamba gari hilo litawasaidia sana Watumishi wa Hospitali ya
Rufaa ya Mkoa wa Singida kuwahi kazini pia litawasaidia kwenye shughuli za misiba ambayo kisheria inapaswa
kusimamiwa na mwajiri. Aidha Daktari Mahenge aliutaka uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida kulisimamia
vizuri gari hilo na kuweka robo ya gharama zilizotumika kulinunua gari hilo kwa ajili ya matengenezo ili hata ikitokea
amekuja Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida baada ya miaka 20 alikute gari hilo likiwa zima.