Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida
(Hospitali ya Mkoa)

Kuagwa kwa watarajali 17 Hospitali ya rufaa ya mkoa Singida

Posted on: November 1st, 2023


Leo tarehe 02.11.2023 Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida imewaaga Wauguzi Watarajali 17 ambao wamemaliza muda wao. Akizungumza katika tafrija hiyo fupi mgeni rasmi Bi Yasinta Alute ambae ni Muuguzi wa Mkoa wa Singida (RNO) aliwaasa Watarajali hao kuishi kwa kuzingatia maadili ya kiuguzi. Pia aliwasisitiza kuwaheshimu na kuwa tayari kujifunza mambo mbalimbali kwa wafanyakazi waliowakuta kazini pindi watakapopata fursa ya kuajiriwa serikalini au katika sekta binafsi. Nae kiongozi wa Watarajali hao waliomaliza muda wao ndugu Nelson aliishukuru menejimenti ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida kwa kuwasimamia vizuri katika kipindi chote walichokuwa hapo Hospitalini na aliahidi kwamba watarajali wote hao 17 watakuwa Mabarozi wazuri wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida.