Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida
(Hospitali ya Mkoa)

MAFUNZO YA HUDUMA KWA WAGONJWA WA DHARURA YATOLEWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA SINGIDA.

Posted on: November 7th, 2023
Akifungua mafunzo hayo ambayo yalifanyika kwa muda wa siku 3, kuanzia tarehe 7.11.2023 hadi tarehe 9.11.2023 Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Viktorina Ludovick alimshukuru Mdau wa Afya KOFIH kutoka Korea kwa kushirikiana na Wizara ya Afya kutoa Mafunzo ya Huduma kwa Wagonjwa wa Dharula kwa wafanyakazi 20 wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida wakiwemo Wauguzi, Madaktari, Wataalam wa Maabara, Wateknolojia Dawa pamoja na Mafundi Sanifu Vifaa Tiba.


Akiongea baada ya Mafunzo hayo Dkt. Wilson Masuke (Mshiriki) amesema, washiriki wote wamejengewa uwezo wa namna ya kunusuru uhai wa wagonjwa mahututi pindi tu wanapofikishwa Idara ya Dharula na Magonjwa ya Nje kwani mgonjwa wa Dharula asipohudumiwa kwa umakini mkubwa pindi anapofikishwa kwenye Idara ya Dharula na Magonjwa ya Nje anaweza kupoteza uhai wake akiwa kwenye korido. 

Nae Kaimu Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida Dkt. David Mwasota wakati akifunga mafunzo hayo na kugawa vyeti kwa washiriki, aliwaambia washiriki kama watayasimamia vizuri yote waliyofundishwa ana imani hakuna mgonjwa wa Dharula hata mmoja atakaekuja kupoteza uhai wake pindi tu atakapofikishwa kwenye idara ya Dharula na Magonjwa ya Nje ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida.