Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida
(Hospitali ya Mkoa)

MGANGA MFAWIDHI SINGIDA RRH AWASILISHA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA BODI YA USHAURI YA HOSPITALI KWA KIPINDI CHA MIAKA MITATU KUANZIA 2019/20 – 2021/22

Posted on: October 17th, 2022

Taarifa hiyo imewasilishwa leo tarehe 19 Oktoba 2022 kwenye kikao cha Bodi ya Ushauri ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida. Katika taarifa hiyo Katibu wa Bodi Dkt. Deogratias G. Banuba ambae ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida amesema kwa muda wa miaka mitatu (3) ambayo Bodi hiyo imetekeleza majukumu yake tangu imechaguliwa na Mhe Waziri wa Afya imefanikiwa kutekeleza mambo mbalimbali katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida ambayo ni :-

  • Kushauri na kuongeza wigo katika huduma za Kibingwa
  • Kuidhinisha Madaktari 10 kwenda kusomea Fani za Kibingwa
  • Kununua Coaster mpya ya Watumishi
  • Kuongeza upatikanaji wa dawa kutoka asilimia 90 – 98% kwa mwaka 2022
  • Kuboresha huduma za Customer Care
  • Kuiwekea Water Dispenser kila idara kwa ajili ya maji ya kunywa
  • Kununua vifaa mbalimbali kwa ajili ya tiba ya viungo na mazoezi
  • Kushauri na kusimamia usimikaji wa mashine za kisasa (CT Scan, Fluoroscopy na Digital X – Ray)
  • Kununua mashine 2 za kisasa kwa ajili ya kutolea dawa ya usingizi wakati wa upasuaji (Universal Anaethesia Machine)
  • Kununua mashine 2 kwa ajili ya matibabu ya Watoto njiti (Phototherapy)
  • Kufanikiwa kuongeza mapato ya Hospitali kutoka shilingi 2,657,838,204.78 mwaka 2019 hadi shilingi 3,287,452,256.33 mwaka 2022
  • Kutengeneza kichomea taka
  • Kuhamisha shughuli za Utawala, Huduma za Meno, Huduma za Macho, Huduma za Wagonjwa wa Nje na Huduma zote za Kibingwa katika majego mapya ya Mandewa
  • Kuhakikisha stahiki na motisha za watumishi zinalipwa kwa wakati kwa kipindi cha miaka 3
  • Kusimamia kikamilifu miradi ya ujenzi inayoendelea Hospitalini kama vile unjenzi wa Nyumba ya Mtumishi, ukarabati wa chumba kwa ajili ya Tiba Mtandao, ukarabati wa vyumba kwa ajili ya CT Scan na Digital X – Ray, ujenzi wa jengo la ICU na EMD, ujenzi wa jengo la Covid – 19 Containment, ujenzi wa Vitako kwa ajili ya kuweka matanki ya kuhifadhia maji safi, ujenzi wa sehemu ya maegesho ya magari, na ujenzi wa sehemu ya kupumzikia ndugu wa wagonjwa (Waiting Bay)

  • Picha ya Basi la Watumishi

  • Picha  ya Kibanda cha Customer Care na huduma    zikiendelea kutolewa.


  • Picha mtumishi akipata huduma ya maji ya chai akiwa    eneo lake la kazi


  • Picha ya vifaa, idara ya Mazoezi kwa ajili ya Tiba ya Viungo

 


Picha ikionesha Mlango wa Chumba cha Digital X-Ray pamoja na Mashine yake 


 

Picha ikionesha Mlango wa Chumba cha Floroscopy pamoja na Mashine yake 


 

 

Picha ikionesha Mlango wa Chumba cha CT SCAN, CT SCAN Machine pamoja na Computer

  • Picha ya “Phototherapy” machine


  • Picha ya jengo la Nyumba ya Mtumishi

  • Picha ya Jengo la EMD ujenzi ukiendelea

 

  • Picha za jengo la Covid-19 Containment

  • Picha ya Ujenzi wa vitako kwa ajili ya kuweka Matanki ya kuhifadhia maji safi kwa matumizi ya hospitali


  • Picha ya sehemu ya maegesho ya magari (Car Parking)

  • Picha ujenzi wa eneo la kupumzikia wagonjwa na ndugu       

  • Picha ya jengo la ICU ujenzi ukiendelea     



  • Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Hospitali Jaji Mstaafu Fatma Massengi akiongoza Kikao cha Bodi

  • Wajumbe wa Bodi Wakifuatilia Kwa Umakini Taarifa ya Utekelezaji wa Majukumu ya Bodi kwa Miaka 3