Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida
(Hospitali ya Mkoa)

MKUU WA MKOA WA SINGIDA AIPONGEZA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA SINGIDA.

Posted on: December 7th, 2021

Pongezi hizo alizitoa tarehe 08/12/2021 alipotembelea banda la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru. Baada ya kupata maelezo kuhusiana na matibabu ya macho, matibabu ya magonjwa ya kina mama na wajawazito, upasuaji wa mifupa, matibabu ya magonjwa ya ndani na huduma ya upasuaji mkubwa na mdogo, Dkt Mahenge alisema Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida inajitahidi sana kutoa huduma bora na zenye viwango kwa wananchi wa Singida pia aliwapongeza watumishi wote wa Hospitali waliofika    Wilaya ya Manyoni kwenye kilele cha miaka 60 ya Uhuru katika Mkoa wa Singida.