MWENYEKITI WA BODI YA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA SINGIDA AUPONGEZA UONGOZI WA HOSPITALI
Posted on: November 30th, 2021Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida Jaji Mstaafu Fatuma Masengi ameupongeza
uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida kwa kutoa Motisha mbalimbali za watumishi katika hospitali hiyo.
Bi Fatuma Masengi ameyasema hayo leo tarehe 30/11/2021 katika kikao cha Bodi ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa
Singida baada ya kupokea taarifa ya watumishi kwa kipindi cha kuanzia Julai 2021 hadi Novemba 2021. Kwa mujibu wa
taarifa hiyo Watumishi wote walioenda likizo kuanzia Julai 2021 mpaka Novemba 2021 wamelipwa pesa zao za likizo na
wengine wanaenda kwa kipindi hiki wanaendelea kulipwa, posho inayotokana na pesa za Bima imelipwa kwa watumishi
wote hadi watumishi wanaojitolea na waliopo mafunzo kwa vitendo wamelipwa, madeni ya likizo, postemoterm, posho ya
masaa ya ziada na posho ya kuitwa kazini ya mwaka 2018/2019 na 2019/2020 yamelipwa, watumishi 84 wamewezeshwa
na Hospitali kuhudhuria mafunzo mbalimbali, watumishi 24 wamehudhuria Makongamano mbalimbali ya kitaaluma na pia
bajeti ya posho ya kujikimu imepanda kutoka 8,500,000/= hadi 12,000,000/= na posho ya masaa ya ziada imepanda
kutoka 8,500,000/= hadi 12,000,000/=.
Mwenyekiti huyo alisema mambo yote haya ambayo wamefanyiwa Watumishi kwa kipindi hiki kifupi ikiwa ni pamoja na
kununuliwa kwa bus ya watumishi aina ya Coaster sio ya kubeza.