NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA ATEMBELEA MIRADI YA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA SINGIDA.
Posted on: February 23rd, 2024Akitembelea miradi mbalimbali ya ujenzi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe amesema serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imedhamilia kwa dhati kuhakikisha wananchi wanapata huduma nzuri na katika mazingira mazuri pindi wanapokwenda kupata matibabu Hospitalini.
Naibu Katibu Mkuu akiongea na Meneja wa Maabara
Pamoja na kutembelea miradi ya ujenzi Dkt. Magembe ametembelea Idara ya Maabara kwa ajili ya kujiridhisha na namna huduma za hospitali zinavyotolewa kwa wananchi. Akiwa katika Maabara ya HRMS Naibu Katibu Mkuu amesema, "Nimefurahishwa sana na kuridhika na huduma za Maabara zinazotolewa katika HRMS nimeona namna ambavyo wataalam wa Maabara wanavyozingatia muda kuanzia kwenye kuchukua sampuli za wagonjwa, kupima hadi kutoa majibu husika".