NAIBU WAZIRI WA AFYA AMPONGEZA MGANGA MFAWIDHI WA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA SINGIDA.
Posted on: January 29th, 2022Naibu Waziri wa Afya, Mhe Dkt. Godwin Mollel leo Januari 29, 2022 amewasili Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida na kufanya ziara ya kukagua shughuli mbalimbali zinazofanywa na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida.
Akiwa katika kibanda cha huduma kwa wateja, Mhe. Dkt. Mollel alimpongeza Mganga mfawidhi kwa ubunifu wa kuweka kibanda cha huduma kwa wateja na alisema kibanda hicho kimejengwa kwa ubora unaotakiwa na amejiridhisha huduma zinazotolewa na kibanda cha huduma kwa wateja Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida ni nzuri. Aidha Dkt. Mollel aliagiza kwamba, Hospitali zote za Rufaa zinapaswa kuwa na Kibanda cha Huduma kwa Wateja.