Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida
(Hospitali ya Mkoa)

Magonjwa ya Ndani

Posted on: April 26th, 2024

Huduma hii huwahusisha wagonjwa wanaosumbuliwa na magonjwa ya ndani. 

Wagonjwa hawa huwa huwa wanaonwa kupitia kliniki husika kwa matibabu. 

Pia huduma ya kulazwa kwa wagonjwa hawa inapatikani kupitia  wodi zetu ambazo  

zimegawanyika katika makundi matatu,

  1.  Wodi ya wanaume (Wodi namba 7)
  2. Wodi ya wanawake (wodi namba 10)
  3. Grade A

RATIBA YA MZUNGUKO WA WODI (WARD ROUND)

SIKU  HUDUMA
JUMATATU MZUNGUKO MKUU 
JUMANNE MZUNGUKO WA KAWAIDA 
JUMATANO MZUNGUKO WA KAWAIDA
ALHAMISI MZUNGUKO MKUU
IJUMAA MZUNGUKO WA KAWAIDA


Wangonjwa wanapopata nafuu huruhusiwa na kupewa tarehe maalumu za kuhudhuria

 kliniki ya kila siku za Jumatano. Aidha huwa tunafanya huduma za kliniki kwa magonjwa 

 mbali mbali kwa ratiba kama inavyoonekana hapa chini.


  •                              RATIBA YA KLINIKI
SIKU        HUDUMA
JUMATATU KLINIKI YA KISUKARI KWA WATU WAZIMA 
JUMANNE KLINIKI YA KISUKARI KWA WATOTO
JUMATANO KLINIKI YA MAGONJWA YOTE YA NDANI
ALHAMISI KLINIKI YA KISUKARI KWA WATU WAZIMA

Note:

  •  Kliniki ya magojwa ya akili hufanyiki kila siku ya wiki.
  • Baadhi ya mgonjwa yanayotibiwa na idara ya magonjwa ya  ndani ni Shinikizo la damu, Kifafa, Pumu, Seli mundu, magonjwa ya moyo na kadhalika.